Daktari aonya kusambaa zaidi kwa COVID-19


0

Daktari wa ngazi ya juu wa magonjwa ya kuambukizwa nchini Marekani, Anthony Fauci  amewaonya maseneta kuwa virusi  vya corona vitasambaa zaidi iwapo nchi hiyo itafungua shughuli zake mapema sana.

Dk Fauci amesema miongozo ya kufungua shughuli za kibiashara tena haitafuatwa na maambukizi madogo madogo yatazua mlipuko ambao maafisa hawataweza kuudhibiti

Akizungumza kwa njia ya video na kamati ya seneti inayoongozwa na chama cha Republican nchini humo, Dk Fauci anasema idadi halisi ya vifo nchini Marekani huenda ikawa kubwa kuliko idadi rasmi inayotolewa.

Maoni yake hayo yanapingana na taarifa iliyotolewa na Rais Donald Trump wa nchi hiyo ambaye anataka shughuli za kiuchumi zifunguliwe tena.

Majimbo kadhaa ya Marekani ambayo tayari yamekwishaanza tena shughuli zao za kiuchumi yana viwango vya juu vya ongezeko la maambukizi ya corona badala ya kushuka.

Ikulu ya White House imeweka miongozo ya kufungua shughuli za kiuchumi kuwa ni jukumu la magavana, kuamua juu ya namna ya kulegeza sheria za kukaa nyumbani zilizowekwa.

Dk Fauci pia amesema kuna chanjo nyingi ambazo zinatengenezwa, lakini hakuna uhakika kama zitakuwa na ufanisi lakini ana matumaini zinaweza 


Like it? Share with your friends!

0