Chadema yapuliza kipenga cha urais


0

TANZANIA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeruhusu wanachama wake kutangaza nia ya kuwania urais, na kwamba kipo tayari kwa majadiliano na vyama vyenye dhamira ya kweli ya kukitoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.

Hayo ameyasema Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, alipozungumza na waandishi wa jijini dar es Salaam leo, akilenga kutoa zaidi kutoa ratiba ya mchakato wa kuchukua fomu za kuteuliwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Kwa mujibu wa Mnyika, mchakato wa kuchukua fomu hizo umeanza leo ambapo watia nia wanatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu hadi ifikapo Juni 15, mwaka huu.

Mnyika anasema mwanachama yeyote anaruhusiwa kuwania kiti hicho, lakini kwa kuzingatia utaratibu mahususi uliowekwa na Chadema.

Amesema utaratibu huo unamtaka mtia nia kuandika barua kwa Katibu Mkuu wa Chadema, ikiambatana na wasifu, kisha Kamati Kuu ndicho chombo chenye mamlaka ya kupitia, kutafakari na kutoa mwelekeo kwa hatua zinazofuata.

Pia, Mnyika anasema ili kuongeza nguvu za kisiasa na ushawishi dhidi ya CCM, Chadema ipo tayari kwa majadiliano na vyama vingine vyenye dhamira ya kushirikiana ili kukiondoa chama hicho tawala kutoka madarakani.

 

 


Like it? Share with your friends!

0