CDC Africa yasema vipimo vya corona Tanzania havina kasoro


0

Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC), kimesema vifaa vya kupimia virusi vya corona nchini Tanzania havina kasoro ya utendaji kazi wake.

Mkuu wa kituo hicho, Dk John Nkengasong, amewaambiwa waandishi wa habari hii leo jijini Addis Ababa, Ethiopia kuwa, ofisi yake inavijua vifaa hivyo, na kwamba vinafanya kazi vizuri.

Shirika la habari la Reuters lililochapisha taarifa limeelezea kuwa viongozi wa serikali ya Tanzania hawakupatikana kuzungumzia tamko hilo, lakini likakumbusha kauli ya hivi karibuni ya Rais John Magufuli kuwa huenda vipimo hivyo vikawa na matatizo.

Africa CDC pamoja na wakfu wa Jack Ma, shirika la msaada la bilionea wa China ndio wasambazaji wa vifaa hivyo.

Kituo hicho kilicho chini ya Umoja wa Afrika (AU) kina majukumu ya kuratibu mapambano dhidi ya mlipuko wa magonjwa barani Afrika.

 

 


Like it? Share with your friends!

0