CCM yaweka kifua mbele kupata ushindi chaguzi za Serikali za Mitaa


0

Siku moja baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutoa taarifa kuhusu uchaguzi mdogo utakaofanyika Juni 17, 2019 na wagombea 29 kati ya 32 kupita bila kupingwa, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hali hiyo inaonyesha wapinzani wanaridhishwa na utendaji wa chama hicho.

Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Kanali Ngemela Lubinga amesema kitendo cha wagombea wa chama hicho kupita bila kupingwa huenda kinaashiria wapinzani wanaridhishwa na utendaji wa chama hicho katika maeneo yao.

“Wananchi wanapewa nafasi ya kuchagua kiongozi wanayemtaka bila kujali vyama lakini kama upinzani wameona aliyechukua fomu wa CCM anatosha ni sawa.” Amesema Kanali Lubinga

Ameongeza kuwa“Hii inaweza kutokana na kuwa vyama vingi vya upinzani bado havijakomaa na wameridhika na utendaji wa CCM kwa kuwa imeshakomaa na imejiimarisha hivyo wanaona hakuna haja ya kuweka mgombea,”.

Hata hivyo, kwa upande wa vyama vya upinzani nchini vimesema kuwa kwa sasa CCM, hawapaswi kujitamba isipokuwa hali hiyo hali hiyo inasababishwa na watu  kuchoshwa  na chaguzi zenye hila na ndiyo sababu wameamua kuacha kushiriki kwa kuwa hakuna jipya watakalolipata.

Kwa muda mrefu sasa vyama vya upinzani vimekuwa na malalamiko kwa Tume ya Uchaguzi, kuhusu namna wanavyoendesha chaguzi nyingi hapa nchini, huku kukiwa na uonevu mkubwa ikiwamo wizi wa kura, kuhakikisha Chama Mapinduzi kinashinda


Like it? Share with your friends!

0