CAG awataka maofisa wake kuwa na misimamo


0

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Profesa Mussa Assad amesema maofisa wa ofisi yake wanatakiwa kufanya kazi kwa kujiamini na kutoogopa chochote pindi wanapotekeleza majukumu yao,  na kuhakikisha wanajibu hoja kwa wakati ili kuonyesha misimamo yao kwenye kazi zao.

Prof. Assad ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua Baraza la Wafanyakazi wa ofisi yake jijini Dodoma, ambapo ameeleza kuwa hakuna sababu ya woga katika utendaji wa maofisa wake, kwani wanapaswa kuwa mfano ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Hata hivyo kwa mujibu wa CAG, kuna baadhi ya mifumo ya kitaalamu zaidi inahitajika katika ukaguzi, mifumo ambayo endapo itapatikana kazi ya ukaguzi itafanyika vizuri zaidi.


Like it? Share with your friends!

0