Bunge laibua upya sakata la uuzaji nyumba za Serikali


0

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeitaka Serikali kurejesha nyumba za umma ilizouza kinyume cha mikataba na malengo ya mauzo.

Msemaji wa kambi hiyo Susan Kiwanga ameyasema hayo bungeni, wakati alipokuwa akitoa maoni yao kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kwa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 20019/2020.

Amesema Serikali imeshindwa kutekeleza azimio la Bunge la kurejeshwa kwa nyumba hizo na pia wabunge wameshaanza hisia  zao kuhusiana na kurejeshwa kwa nyumba hizo.

“Kambi Rasmi ya Upinzani inarudisha tena ombi kutaka Serikali ya Awamu ya Tano kuzirejesha nyumba za Serikali, ambao hawakustahili na zoezi zima lililogubikwa na rushwa na upendeleo mkubwa wa kiundugu na uchafu mwingine wa aina hiyo,” amesema Kiwanga

Amesema kwa kuwa awamu ya tano ni Serikali ya kunyoosha nchi, itakuwa ni vyema ikanyoosha pale ambapo hapakuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria.

“Kambi ya Upinzani inauliza ni lini Takukuru itachukua nafasi yake katika hili,” amehoji Kiwanga.

 

 


Like it? Share with your friends!

0