Nyota wa Star Wars John Boyega apanda chati kupinga ubaguzi wa rangi


1
1 point

MAREKANI

Baadhi ya waongozaji na watayarishaji wa filamu nchini Marekani, wamemsifu mcheza filamu maarufu wa Hollywood na nyota wa filamu ya Star Wars, John Boyega kushiriki maandamano ya kudai haki za watu weusi ya London nchini Uingereza siku ya Jumatano.

 

Boyega akiwa na kipaza sauti mbele ya waandamanaji wengine, ametoa hotuba inayovuta hisia za waandamanji na kutawala katika mitandao ya kijamii.

Amesema maisha ya watu weusi yana umuhimu kila wakati hivyo inahitaji kila mtu aelewe ni kwa namna gani mambo ya ubaguzi yanaumiza.

Boyega anayasema hayo akiamini kwamba yanatoka moyoni mwake pasipo kujali kama atapoteza kazi yake ya uigizaji au laa; lakini hatojali chochote.

 

Hata hivyo, kauli yake imewavutia baadhi watayarishaji na waongozaji wa filamu wa Hollywood, Marekani walioonesha kumuunga mkono.

Muongozaji wa filamu ya Get Out na mshindi wa tuzo ya Oscar, Jordan Peele kupitia ukurasa wa twitter akasema kuwa wapo pamoja naye.

Naye mwandishi wa filamu za Harry Porter JK Rowling, ameandika, “nitafurahi kufanya kazi na wewe muda wowote.”

 

Mtayarishaji wa filamu za Star Trek na Star wars naye hakuacha kutoa ya moyoni juu ya Boyega, ameandika kuwa “kama nitaendelea kufanya kazi, daima nitakuomba tufanye kazi na wewe, heshima na upendo tele kwako.”

Boyega ameshiriki maandamano hayo kuonesha hisia zake juu ya kifo cha Mmarekani mweusi, George Floyd aliyefariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi Mei 25, mwaka huu katika jimbo la Minnesota nchini Marekani

 

 

 


Like it? Share with your friends!

1
1 point