BoT yafungia maduka ya kubadilisha fedha


0

Baada ya sintofahamu kufuatia zoezi la kufungwa kwa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, linalotajwa kuendelea katika jiji la Dar es salaam, Benki Kuu ya Tanzania imesema zoezi hilo limefanyika kwa mujibu wa sheria ya masuala ya fedha, na kwamba imefanya hivyo baada ya kubaini kuwa kuna baadhi ya maduka yanfanya biashara hiyo kinyume cha sharia hiyo ikiwamo udanganyifu.

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw Jerry Sabi. Amesema kufuatia ukaguzi huo, Benki Kuu ya Tanzania imeanza utaratibu wa kufuta leseni za maduka yote yaliyokutwa yanaendesha biashara hiyo bila kuzingatia masharti ya leseni, na mfanyabiashara yeyote atakayekutwa anaendesha biashara hiyokinyume na sharia basi sharia itachukua mkondo wake.

“Mnamo mwezi Desemba mwaka 2018, Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini kote na kubaini kuwa mengi hayakidhi matakwa ya kisheria ya biashara hiyo. Hivyo, iliyaandikia maduka hayo kuyataka kutoa maelezo kwa nini yasifutiwe leseni kutokana na ukiukaji huo. Hatua zilizochukuliwa jana zinatokana na tathmini ya taarifa ambazo Benki Kuu ya Tanzania ilizipokea kutoka kwa waendeshaji wa maduka hayo.” Amesema Jerry Sabi

Ni takribani mwezi mmoja sasa tangu maduka ya kubadilisha fedha ya jijini Arusha kufungwa, zoezi ambalo lilibua hisia tofati kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara, huku wengi wao wakiathirika kiuchumi.

Hata hivyo katika taarifa ya Benki Kuu, imeendelea kuutahadharisha umma kutotumia huduma zisizo rasmi za ubadilishaji wa fedha za kigeni, kutokana na hatari mbalimbali ikiwemo kuibiwa au kupewa fedha bandia.

 

.


Like it? Share with your friends!

0