Beijing yafungwa corona ikilipuka upya China


0

BEIJING

Jiji la Beijing limeweka upya amri ya kutotoka nje na kufanya vipimo vya COVID 19 kwa wananchi, baada ya China kuripoti idadi ya juu ya maambukizi ya kila siku ya virusi vya corona huku kukiwa na hofu ya kutokea kwa wimbi la pili la mlipuko wa ugonjwa huo.

Mji mkuu huo wa China umeripoti visa vipya 36 vya maambukizi hayo leo, na kufanya jumla ya visa hivyo kufikia 79 tangu ilipoanza kuripotiwa kwa mara ya kwanza Juni 12, mwaka huu, ikiwa ni baada ya miezi miwili kupita bila maambukizi nchini humo.

Wimbi jipya la maambukizi hayo linatajwa kuwa limeanzia kwenye soko la jumla la vyakula ambalo ndio wasambazaji wakubwa wa matunda, mboga mboga, nyama na vyakula vya baharini katika mji huo.

Soko hilo limefungwa tangu jumamosi, ikiwa ni jitihada za kuzuia kuenea kwa maambukizi hayo yameripotiwa kwenye majimbo ya Liaoning na Hebei yenye visa vipya vitano.

Vyombo vya habari vya serikali ya China vimekuwa vikielezea kwa wananchi hatua madhubuti za kuchukua ili kuzuia maambukizi kuenea zaidi.

 


Like it? Share with your friends!

0