Bei ya Mafuta yahofiwa kuongezeka duniani


0

Vyombo vya habari vinavyojishughulisha na masuala ya uchumi duniani kama vile gazeti la Financial Times na televisheni ya CNBC vimesema kuwa, huenda bei ya mafuta ikapanda vibaya kwa hadi dola 10 kwa pipa, baada ya ndege zisizo na rubani za jeshi la Yemen kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya taasisi kubwa zaidi ya mafuta a Saudi Arabia.

Shambulio la ndege 10 zizizo na rubani za Jeshi na Kamati za Kujitolea za Wananchi wa Yemen limeilazimisha Saudi Arabia kukata nusu nzima ya uzalishaji wake wa mafuta.

Taarifa rasmi kutoka Serikali ya Saudi Arabia inasema kuwa nchi hiyo imepoteza uwezo wa kuzalisha mapipa milioni tano na laki saba kwa siku, yaani nusu nzima ya uzalishaji wake. Hata hivyo wataalamu wa mambo wanasema kuwa, bado ni mapema mno kujua hasara hasa iliyopata Saudi Arabia kutokana na shambulio hilo ambapo hasara hizo zinaonekana ni kubwa mno ikilinganishwa na takwimu zinazotolewa na Serikali ya Saudia.

Mkuu wa taasisi ya mafuta la Lipow Pil Associates ya Marekani, Andrew Lipow, amesema kuwa, suala hili ni kubwa sana na huenda kukawa na hali mbaya zaidi kutokea katika soko la mafuta. Huenda bei ya mafuta ikapanda kwa baina ya dola 5 hadi 10 kwa pipa, yaani baina ya silimia 12 hadi 25 ya bei ya mafuta kwa kila geloni moja duniani.

Kwa upande wake, gazeti la Financial Times limesema kuwa, Wakala wa Kimataifa wa Nishati, jana Jumapili umetoa taarifa kuhusu shambulio hilo na kusema kuwa, unaendelea na mazungumzo na wazalishaji wakuu wa mafuta duniani ili kuziba pengo lililosababishwa na kusimamisha Saudi Arabia kuzalisha nusu ya mafuta yake kwa siku.

 


Like it? Share with your friends!

0