AU kuchunguza dawa ya mitishamba ya Madagascar


0

Umoja wa Afrika (AU) upo kwenye  mazungumzo na utawala wa Madagascar, kupata maelezo ya kisayansi kuhusu usalama na ufanisi wa dawa ya mitishamba iliyotangazwa hivi karibuni kuwa inazuia na kutibu COVID -19.

Aprili 30, mwaka huu, Kamishna wa Tume ya Umoja wa Afrika inayohusika na masuala ya kijamii, Amira Eif Adil, alifanya mazungumzo na Balozi wa Madagascar nchini Ethiopia, Eric Randrianantoandro na kuafikiana kuwa nchi wanachama watapewa maelezo muhimu kuhusu dawa hiyo.

Baada ya kupata maelezo, Umoja huo kupitia kituo cha udhibiti wa magonjwa cha Marekani katika ukanda wa Afrika (Africa CDC), kitatathimini taarifa zilizokusanywa kuhusu usalama na ufanisi katika tiba dhidi ya virusi vya corona.

Hata hivyo, AU imesema kuwa tathimini yake ya madawa ya mitishamba itazingatia maadili ya kisayansi duniani, katika kukusanya ushahidi muhimu kuhusu ufanisi wa mitishamba.

Hatua hii inakuja baada ya Rais Andry Rajoelina wa Madagascar kushiriki kikao cha AU cha wakuu wa nchi, ambapo aliwafahamisha kuhusu dawa hiyo anayoamini inazuia na kutibu virusi vya corona.


Like it? Share with your friends!

0