Android 11 Beta sasa inapatikana kwenye simu za OnePlus 8


1
1 point
OnePlus 8

  Tangu uzinduzi toleo la beta la Android 11 lilipatikana kwa wamiliki wa simu za Pixel tu, ila sasa itapatikana kwenye simu za OnePlus pia.  Hii inaoneshana wazi kuwa awali, kampuni ya Google ambao ndio wamiliki wa vifaa vya Pixel na waendelezaji wa Android walikuwa na mpango wa kujipendelea.

Android 11 Beta sasa imeanza kupatakina  kwenye vifaa vingine. Kwenye chapisho la mtandaoni, OnePlus wametangaza kuwa walifanya kazi ya ziada kuhakikisha toleo hilo jipya la Android linapatikana kwa watumiaji wa simu za OnePlus 8.

Kampuni hiyo chipukizi inayoleta tishio kubwa la upinzani katika soko la simu janja iliweka kiungo kinachowawezesha watumiaji wa simu za OnePlus 8 na OnePlus 8 pro kupakua mfumo mpya wa Android 11.

Android Google Pixel 4

Licha ya kuweka kiungo tu, kampuni ya OnePlus iliambatanisha onyo kali kwa watumiaji wake kuwa mfumo huo mpya haufanyi kazi kwa ufasaha na bado unafanyiwa maboresho  na kuna baadhi ya huduma hazitakuwepo kama vile kufungua simu kwa uso, OK Google na simu za video. Na ili kuhakikisha kuwa watumiaji wake wanapata nafasi ya kurudisha Android toleo la nyuma kama hawatoridhika na Android 11, kampuni ya OnePlus imeambatanisha na kiungo cha kupakua Android 10.

Moja ya sifa kubwa za Android 11 ni muonekano wa maputo na maduara yanayofanania na mfumo wa Facebook ambapo chati zinaonekana juu ya program zingine kama maputo na kufanya iwe rahisi kufungua tena mara mtumiaji atakapopokea ujumbe. Android 11 pia imeongeza widget ya kuendesha media kwenye sehemu ya setting za haraka yani Quick Settings inayopatikana unapogusa na kushusha chini kutoka sehemu ya juu ya kifaa chako – maarufu kama Slide down Bar. Pia mfumo huu mpya umeongeza mapendekezo ya programu za kutumia kwenye mstari wa mwisho wa home screen punde tu mtumiaji anapoifungua. Mfumo huu utapatikana kwenye vifaa vingine hapo baadaye lakini kama utahitaji kuutumia kwa sasa utalazimika kutumia vifaa vya Pixel au OnePlus 8 na OnePlus 8 Pro.

Kuna watumiaji zaidi ya bilioni 3.5 wa simu janja duniani kote na kati ya watumiaji hao, watumiaji zaidi ya 8 kati ya 10 wanatumia simu za Android, Hii  ina maana kuwa katika kila simu kumi (10) zinazouzwa duniani kote simu 8 au zaidi zinatumia mfumo wa Android.


Like it? Share with your friends!

1
1 point