Amuua mwanaye kwa kisu


0

Mkazi wa Kijiji cha Katangara Wilayani Rombo, Philipina Donath(37) amedaiwa kumuua mtoto wake wa miaka mitano kwa kumkata na kisu shingoni kisha kujisalimisha mwenye kituo cha Polisi.

Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kilimanjaro Hamis Issah amesema leo Septemba 2019 kuwa tukio hilo lilitokea jana katika Kijiji cha Katangara Mashati.

“Cha kushangaza mwanamke huyo baada ya kufanya mauaji ya mwanaye alijisalimisha mwenyewe  kwenye kituo cha Polisi Mashati na Polisi walipofika nyumbani kwake walikuta mwili wa mtoto huyo ukiwa chini huku pembeni mwa mwili huo kukiwa na kisu chenye damu, “amesema Kamanda Issah.

Amesema mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika Hospitali  ya Wilaya ya Huruma kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 


Like it? Share with your friends!

0