Afya ya Kabendera yalenta gumzo mahakamani


0

Mwandishi wa habari Erick Kabendera ameiambia Mahakama jana  kuwa anapata maumivu makali ya paja na mfupa wa mguu wa kulia huku upelelezi wa kesi yake ukitajwa kuwa bado haujakamilika.

“Hakuna vifaa walinipima damu na kunichoma sindano tatu, tatizo likapotea kwa muda lakini kwa siku nane zilizopita ninapata maumivu makali ya paja na mfupa,” amesema Kabendera.

Wakati akiwasilisha hoja yake mbele ya Hakimu Rizwile, Wakili wa Kabendera Jebra Kambole amesema Kabendera ni mgonjwa na sasa anashindwa kutembea Kwani mguu wake wa kulia  umepooza na bado anapata shida ya kupumua nyakati za usiku mpaka sasa hajapatiwa matibabu sahihi.

“Tumeeleza hii hoja ni wiki ya pili sasa tunaiomba Mahakama itoe msisitizo juu ya hili na kuielekeza Jeshi la Magereza limpe fursa Kabendera kutibiwa na tupewe taarifa rasmi kuwa anaumwa nini,”Wakili Jebra Kambole

Aidha Wakili wa Serikali Wankyo Simon  ameiambia Mahakama kuwa  upelelezi wa kesi ya uhujumu Uchumi inayomkabili Erick  Kabendera bado haujakamilika, katika baadhi ya maeneo lakini alishindwa kuiambia Mahakama ni maeneo gani ambayo bado.

Aidha Hakimu Augustine  Rwizile ameiharisha kesi hiyo hadi Septemba 18, itakapotajwa tena na kumataka Kabendera kukutana na daktari wake siku ya kesho na kuja kujieleza Mahakama kinachoendelea kuhusu afya yake pale kesi yake itakapotajwa tena.

Erick Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo Kujihusisha na genge la uhalifu, Kukwepa Kodi kiasi Cha Shilingi Milioni 173,247,047.02, na utakatishaji Fedha Makosa ambayo hayana dhamana.Kabendera alikamatwa nyumbani kwake Mbweni mnamo Julai 29 Mwaka huu.

 


Like it? Share with your friends!

0