“Acheni kuichukia serikali”- Dk.Tulia Ackson


0

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson amesema wapo watu wana chuki na Serikali bila kujua, kisha chuki hiyo wanawaambukiza watoto wao.

Amesema hayo leo kwenye kongamano la amani linalofanyikia kwenye Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu sabasaba jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Dk Tulia amesema taifa bora ni lile linalolinda na kuthamini amani na kuthamini uhuru wa wengine pasi na kuwaumiza wengine.

Amesema uhuru wa mtu unaishia kwenye pua yake na ukizidi hapo unamuumiza mtu mwingine kwa kumfanya akose amani binafsi na kuiweka nchi kwenye taharuki.

“Tunataka nchi ikue zaidi kwenye taswira ya viwanda tusingependa watu wanaochochea machafuko” amesema.
Amefafanua miongoni mwa wananchi wapo wanaovunja amani na hawataki nchi iwe na amani.

“Tujiepushe na hayo ili tusitumbukie kama taifa kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani, tuna nafasi ya kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa amani,” amesema.

Dk Tulia amewaasa kwenye jukumu la kuhudumia wananchi wawahudumie kwa namna ambayo hawatakosa amani.


Like it? Share with your friends!

0