Acacia yalimwa faini nzito ya 5.6 bln


1
1 point

Serikali imeupiga faini ya shilingi bilioni 5.6, mgodi wa dhahabu wa Acacia North Mara, kwa kosa la kutiririsha maji yenye kemikali kwenye makazi ya watu, vijito na mito.

Uamuzi huo ulitangazwa jana mjini Tarime na Mkurugenzi wa Baraza la Mazingira (NEMC), Dk. Samuel Gwamaka mbele ya mawaziri January Makamba, Waziri wa Mazingira na Dotto Biteko, Waziri wa Madini, ambao walifika hapo kwa lengo la kukagua mifumo ya kudhibiti na kuhifandhi maji taka ya mgodi huo.

Pamoja na faini hiyo, pia mgodi huo umepewa wiki tatu urekebishe kasoro zilizobainika katika bwawa lake la kuhifadhi maji taka yenye sumu, ambayo uchunguzi wa kitaalam umethibitisha yanavuja na kuingia kwenye makazi ya watu na kuathiri maisha yao na mazingira kwa ujumla.

Kwa upande wa mawaziri hao, wamesema nia ya Serikali si kuwaadhibu, kuwapiga faini au kufungia shughuli za uwekezaji, lakini kilichowasukuma kuchukua hatua hizo ni kulinda maisha ya wananchi, mazingira lakini pia kusimamia sheria na masuala ya usalama. 


Like it? Share with your friends!

1
1 point