100 waopolewa kwenye machimbo


0

MYANMAR

Miili ya watu zaidi ya 100 ya wachimba madini katika mgodi wa Jade wameopolewa kutoka kwenye tope baada ya maporomoko ya ardhi kutokea kaskazini mwa Myanmar hii leo
Hiyo ni mojawapo ya ajali mbaya kuwahi kuikumba sekta hiyo nchini humo.
Mkasa huo umetokea baada ya mvua kubwa kunyesha karibu na mpaka wa China katika jimbo la Kachin.

Idara ya Zimamoto ya Myanmar, imesema wachimba madini hao walifunikwa na tope kubwa na mpaka sasa miili ya watu 113 imepatikana.
Polisi wa eneo hilo wamesema waathiriwa walikaidi onyo la kutofanya kazi katika migodi hiyo wakati wa mvua.
Shughuli ya utafutaji na uokozi imesitishwa kwa muda kwa sababu ya mvua kubwa.
Watu hufariki kila mwaka wakati wakifanya kazi katika sekta hiyo yenye faida kubwa, lakini isiyodhibitiwa ipasavyo ya madini ya jade.

Sekta hiyo inawatumia wafanyakazi wahamiaji wanaopewa malipo duni kuchimba madini hayo yanayothaminiwa sana nchini China.

 


Like it? Share with your friends!

0